Fataki
za kumulika
Shirika
la Arasan Match Industries lilifikia daraja za juu kabisa za mafanikio katika
uundaji wa fataki, baruti ndogo, fataki za kumulika, virembesho na baruti za kurusha
angani. Fataki zetu za aina mbalimbali zinafahamika kwa usalama wake na pia kwa
jinsi wanavyoridhika wateja wetu. Tumeweza kufanya maendeleo na uvumbuzi wa hali
ya juu kabisa katika shughuli za fataki.

Tuna
uwezo wa kutengeza fataki za maagizo maalum (specialty), zinazotumika kwa mahitaji
maalum. Pia, huenda kuwa sisi ndio watengezaji wa pekee wanaosafirisha vishtua
ndege yaani baruti ndogo zenye kushtua ndege mashambani, hadi mataifa ya ng'ambo.
Usalama ni jambo la umuhimu mkubwa zaidi kwetu katika Shirika la Arasan Match
Industries. Kila moja kati ya fataki zetu hufanyiwa majaribio ya viwango vya juu
zaidi vya usalama, ili matumizi yake ya baruti yawe imara na salama. Tunafwatilia
pia kanuni sawa za usalama wakati wa utengezaji.
Moyo
wetu wa kujihimiza kufanya uvumbuzi umetuwezesha kuunda aina mbalimbali mpya za
fataki. Tuna kila aina ya fataki kwa mahataji yako ya sherehe za aina tofauti,
jambo hili limefanya Shirika la Arasan Match Industries kuwa suluhisho kamili
la mahitaji yako yote.
Arasan
Gift Boxes